Rozari Takatifu

Rozari.

Mama kanisa kwa namna ya pekee anatualika sote kujumuika kwa pamoja kusali rozari takatifu hasa kipindi hiki maalmu kilichotengwa na kanisa kuenzi na kusali rozari takatifu kwa moyo mkuu. Lengo likiwa ni kutuimarisha kiroho, kutusogeza karibu na toba na wongofu, kukua katika fadhila, ulinzi dhidi ya majaribu na kupokea rehema kwa dunia nzima pamoja na mambo yetu binafsi kadri ya mahitaji yetu.

Katika kulitambua hilo, parokia ya imeandaa utaratibu maalumu ambapo kila siku kwa mwezi mzima wa 10 (kuanzia tarehe 1/10/2025 Hadi 31/10/2025) kutakua na Ibada ya rozari takatifu kuanzia saa 11:00 jioni. (kwa siku za Alhamisi ibada ya rozali itaanza saa 10:00 jioni).

1. Matendo ya furaha( Jumatatu na Jumamosi)

2. Matendo ya Mwanga (Alhamisi)

3. Matendo ya Huzuni (Jumanne na Ijumaa)

4. Matendo ya utukufu (jumatano na jumapili)

Kusali rozari ni Ibada inayotuunganisha sisi na Yesu kristu kupitia kwa Mama Bikira la Maria. Mtakatifu Luis Maria Grignion wa Montfort analisisitiza Hilo kwa kusema “rozari ni silaha yenye nguvu unayotuwezesha kuushika moyo mtakatifu wa Yesu.”

Leave a Reply