Uongozi na Uangalizi

Parokia ipo chini ya uongozi wa mtakatifu mlinzi Mt. Fransisko Ksaveri, parokia hii inaongozwa na mapadre wajesuiti wa kanda ya Afrika mashariki na viongozi wa kanisa wanaojitolea na kujitahidi kila siku kuimarisha na kukuza imani katoliki ya waumini wote parokiani. Wanaviongozi wa parokia wanatambua na kuwajibika kama wabatizwa waliozaliwa upya ndani ya Kristo na kwa Roho Mtakatifu katika kuutangaza na kuusimika Ufalme wa Mungu katika jumuiya zote za parokia ya Mt. Fransisko Ksaveri.
Tunaamini katika kukuza imani itakayowawezesha waumini kuwa na mahusiano ya karibu zaidi na ya kibinafsi na Mungu Mwenyezi. Kwa kufanya hivyo, tunalenga kuwawezesha waumini wetu kuimarika kiroho na kuwa na mtazamo chanya kuhusu maisha yao na wengine.
Tunatarajia kuwa utafurahia na kufaidika na huduma zetu na kujihusisha katika jamii yetu ya parokia.
