UTUME WA KATEKESI MASHULENI
Parokia yetu ya Mtakatifu Fransisko Ksaveri inashiriki kikamilifu katika uinjilishaji mashuleni ambapo Baba Paroko anahimiza sana kuhusu umuhimu wa kuwafundisha watoto dini wakiwa katika umri mdogo. Mafundisho ya Katekesi yanawasaidia wanafunzi kuanzia shule za msingi hadi sekondari. Kufikia mwishoni mwa mwaka jana 2024 tumeweza kuzifikia shule zote zinazozunguka parokia yetu. Kulingana na taarifa ya mwaka jana shule nyingi zimekuwa na mwamko mkubwa katika mafundisho ya Katekesi na somo la dini kwa ujumla wake. Wanafunzi wengi walifaulu vizuri katika mtihani wa dini unaotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kwa ngazi zote yaani shule za msingi na za sekondari. Kwa ujumla mafundisho ya dini mashuleni yaameleta hamasa kubwa hasa katika kufundisha maadili ya Kikristo na hivyo kufanya wanafunzi wawe na hofu ya Mungu na kuwaheshimu wanadamu wenzao.
Wanafunzi wa shule ya msingi Nyanshana wakiwa kwenye darasa la katekesi.