Ibada na Misa

Ibada za Misa: Misa ni kitovu cha ibada katika Kanisa Katoliki, na parokia yetu inaendesha misa kwa siku zote za wiki ili waumini waweze kushiriki katika Ekaristi Takatifu. Misa hizi ni nyakati muhimu za maombi, tafakari, na ushirika na Mungu kupitia Neno na Ekaristi.

Ibada Maalum: Mbali na misa za kawaida, parokia yetu inaandaa ibada maalum kama vile ibada za Novena, Misa za Shukrani, na ibada za kuombea wagonjwa. Ibada hizi ni fursa muhimu kwa waumini kushiriki katika maombi ya pamoja na kupokea baraka za Mungu kwa njia maalum.

Kitubio/Maungamo

Sakramenti ya Kitubio: Kitubio, pia kinacho julikana kama maungamo, ni sakramenti muhimu ambapo waumini wanatubu dhambi zao na kupokea msamaha kutoka kwa Mungu kupitia kwa kuhani. Parokia yetu ina ratiba maalum za kitubio ambapo waumini wanaweza kumwendea kuhani kwa ajili ya kitubio. Maandalizi ya Kitubio: Tunatoa mafundisho na maandalizi kwa waumini, hasa watoto na vijana, ili kuhakikisha wanajua umuhimu wa sakramenti ya kitubio na jinsi ya kujiandaa vizuri kwa ajili ya kitubio.