Miongoni mwa matukio yenye kugusa maisha ya waumini, parokia imeendelea kutoa nafasi za kuwaimarisha wanandoa, wazazi na vijana walio katika hatua mbalimbali za maisha.

Kwa njia ya mafundisho, ushauri wa kiroho na sala za pamoja, familia zimepata fursa ya kutafakari wajibu wao wa kujenga nyumba zenye upendo, msamaha na maelewano. Tukio hili lilionesha wazi kuwa familia ni msingi wa Kanisa na jamii, na kwamba malezi bora huanzia nyumbani.

Waamini walihimizwa kudumisha maombi ya kifamilia, mawasiliano mema, na moyo wa kusaidiana katika changamoto na mafanikio. Hii ni hatua muhimu katika kuijenga parokia iliyo imara kuanzia ngazi ya familia.
